Takwimu zinaonesha kuwa, mawigi sita kati ya kila mawigi kumi ya nywele yanatoka Xuchang, Mkoa wa Henan wa China, ambao pia unajulikana kwa jina la “Mji Mkuu wa Mawigi Duniani.” Mawigi yanayozalishwa na Kampuni inayojulikana sana ya Rebecca siyo tu ni maarufu sana nchini China, bali pia katika masoko ya nje ya China, hasa katika mabara ya Amerika na Afrika.
Mkuu wa Kampuni ya Mauzo ya Chakula ya Slavs tawi la Urumqi Krasik Pavel akiuliza sera kuhusu biashara kwenye Kituo cha Huduma kwa Kampuni za Kigeni cha Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia la Urumqi. (Picha na Han Ting/People’s Daily Online) “Kuna fursa nyingi hapa Xinjiang, zikisubiria wawekezaji mwafaka kuzigundua,” anasema Hendrik Sybrand Alblas, mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Usafirishaji ya Alblas ya Uholanzi.
Ni kwa namna gani kipande cha chuma kinageuka kuwa gari zima? Kiwanda cha Kampuni ya Magari ya BYD kilichopo mji wa Zhengzhou wa Mkoa wa Henan, China kiko hapa kujibu maswali yako. Hebu tuingie ndani ya kiwanda hicho pamoja na timu ya utafiti ya waandishi habari wa People’s Daily Online ya “China Inayosonga Mbele” na kutazama pamoja namna magari yanavyoundwa.
Eneo la ufugaji wa samaki wa samoni la Xinjiang Tianyun. (Picha na Li Xinyang/People’s Daily Online) Katika muongo uliopita, samaki wa samoni wa tani nyingi “wameogelea” kutoka Wilaya ya Nilka ya Eneo linalojiendesha la Kabila la Wakazakh la Ili, Mkoa wa Xinjiang wa China kwenda katika nchi nzima ya China na sehemu mbalimbali duniani.