Jioni ya Mei 26, Soko la Sanaa za Ubunifu katika Mtaa wa Utamaduni na Ubunifu wa Taoxichuan mjini Jingdezhen, Mkoa wa Jiangxi wa China, lilikuwa limejaa watu. Vibanda vya bidhaa zaidi ya 400 vilikuwa vimepangwa kwa mstari mrefu, na vyombo vya kauri vinavyoonesha ubunifu wa aina mbalimbali vilivutia watalii kusimama na kuchagua.
Mapema katika msimu wa joto, wakati anga linaanza kuwa giza, kando ya Barabara ya Wulin mjini Hangzhou, China, safu kadhaa za mabanda ya maduka huwekwa kwenye mtaa huo wenye urefu usiofikia kilomita 1, na wafanyabiashara wenye mabanda hayo hukaribisha wateja kwa shauku na ukarimu chini ya mianga mizuri ya taa, na “maisha mazuri ya usiku” ya Hangzhou yanaanza hapa. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mji huo imetilia maanani sana maendeleo ya uchumi wa usiku na umezalisha kwa mafanikio mfululizo wa chapa za uchumi wa usiku kupitia uungaji mkono wa sera na uboreshaji wa mazingira ya biashara.
Wakati wa jioni, ukitembelea kwenye Soko la Enzi ya Tang la uwazi wa usiku kucha, unaweza kuona watu wengi wanaovaa mavazi ya kijadi ya China wakipiga picha karibu na ukuta mwekundu. “Nahisi kama nimepita katika wakati wa enzi ya zamani! Nataka kurekodi urembo wangu kwenye hali nzuri ya jioni ya “Mji wa Chang’an (uliokuwa Mji Mkuu wa China katika Enzi ya Tang) ”.