Lugha Nyingine
Maelezo ya pili ya picha ya katuni kuhusu uhalifu wa Marekani wa kutunga habari iliyoitwa ukweli wa mambo ili kupinga mpinzani:Kuzusha“tukio la Ghuba ya Beibu” ili vita vipambe moto
Agosti 4, mwaka 1964, rais wa Marekani wa wakati huo Johnson alitoa hotuba akijidai kuwa manowari ya Marekani ilishambuliwa na mizinga ya manowari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam katika Ghuba ya Beibu siku hiyo, hivyo ilitokea migorogoro ya kijeshi kati ya pande hizi mbili. Badaaye, Bunge la taifa la Marekani lilipitisha ati "Azimio la Ghuba ya Beibu" na kumkubali Johnson achukue hatua husika dhidi ya "shambulio hilo."
Lakini, “Tukio la Ghuba ya Beibu”kabisa ni uzushi tu . Mwaka 2005, Idara ya Usalama ya kitaifa ya Marekani ilitoa ripoti kukiri kuwa Agosti 4, mwaka 1964 kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kutokuwepo kwa manowari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam karibu na manowari ya Marekani. Kutokana na kumbukumbu kwenye faili za jeshi la wanamaji la Marekani, manowari mbili za kulinda meli nyingine zilipiga mabomu ya mizinga karibu 400 na mabomu matano kwenye maji ya kina kirefu, lakini kwa kweli mabomu hayo yalikuwa hayakuwa na malengo kabisa. Rubani aliyetekeleza jukumu usiku huo James Stockdale alikumbuka kuwa wakati huo manowari yao yalikuwa yanapiga mabomu kwa malengo waliyofikirika tu , ambapo hakuwepo mizinga ya manowari, isipokuwa giza totoro na mabomu yaliyopigwa ya manowari ya Marekani, hakuwa na chochote kingine.
Hata kama kulikuwa hakuna“Tukio la Ghuba ya Beibu”, Marekani ilikuwa inaweza kutafuta kisingizio kingine kipya kwa kuingilia kati vita hivyo. Kwa kuwa lengo halisi la Marekani ni kuendelea na umwamba wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma