Lugha Nyingine
Katuni: Kupanga mpango wa “Msitu wa Kaskazini” na kuotea kushambulia nchi nyingine
Mnamo mwaka 1959, Fidel Castro aliongoza jeshi la uasi kupindua utawala wa kidikteta wa Cuba uliopendelea Marekani, na kuanzisha serikali ya mapinduzi. Serikali ya Marekani ilifanya chini juu ili kumwangusha Castro.
Mpango wa “Msitu wa Kaskazini” ulifichuliwa mwaka 1997, ambao kiini chake ni Marekani kufanya “mashambulio mfululizo ya kigaidi” dhidi ya mambo ya kijeshi na wananchi wake, halafu kuishtaki serikali ya Cuba kwa vitendo hivi vyote, ili kupata kisingizio cha kushambulia Cuba. Mpango wa “Msitu wa Kaskazini” ulihusisha kuteka nyara na kuangusha ndege za Marekani, kubomoa meli za Marekani na kupanga matukio ya kigaidi kwenye miji ya Marekani. Kwa bahati, mipango hiyo haikuidhinishwa mwishowe.
Ili kudumisha umwamba wake, Marekani ilifika hadi kutunga mpango wa kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi yake yenyewe, ili kupata uungaji mkono na wananchi wake, vitendo hivyo viovu kabisa labda vinavyoweza tu kufanywa na Marekani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma