Lugha Nyingine
Katuni: Marekani yasema uwongo kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kutumia “sabuni za unga”
Mwaka 2003, Marekani ilianzisha vita vya Iraq kwa kisingizio cha Iraq kuficha “silaha za mauaji ya halaiki” na kuunga mkono wagaidi kisiri.
Tarehe 5, Februari, mwaka 2003, waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati huo Jerome Powell alitoa neli moja la jaribio lililojazwa na unga mweupe, na akidai kuwa hii ni “silaha ya mauaji ya halaiki” inayotafitiwa na kutengenezwa na Iraq. Rais Putin wa Russia alipozungumzia jambo hilo mwaka 2014 alisema, “Kitu kisichojulikana ndani ya neli hiyo labda ni sabuni za unga.” Powell alipohojiwa na vyombo vya habari vya Marekani alisema, “Nilionesha ushahidi kwa dunia nzima nikiwa kwa niaba ya Marekani, jambo hilo litakumbukwa nami daima. Sasa ninaona uchungu sana.”
Marekani ilitegemea kisingizio cha neli moja ya “sabuni za unga ”, kushirikisha nchi za muungano wake bila kutoa ripoti kwa Umoja wa Mataifa ikavamia Iraq kwa upande mmoja, na kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya migogoro kwa muda mrefu, ambapo watu laki 2 hadi laki 2.5 hivi walikufa katika vurugu za vita.
Hii ni njia ya Marekani ya kudanganya wazi kwenye muktadha wa kimataifa. Kisingizio kisicho na mantiki kimeonesha kwa dunia nzima sura yake ya “kiovu”. Vitendo hivyo vya Marekani visivyowajibika si kama tu vimedhuru vibaya watu wasio na makosa yoyote, bali pia vimezifanya “demokrasia na haki za binadamu” ilizojenga Marekani kwenye msingi wa ubinafsi wake ziwe upuuzi wa kuchekesha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma