Lugha Nyingine
Marekani aliye mhusika kwenye msukosuko wa Ukraine:
Kutia mafuta kwenye moto bila kusita, kuhamisha migongano na kuipaka China matope
Mchoraji wa picha ya katuni: Ma Hongliang
Katika suala la Ukraine, upande wa China unashikilia msimamo wa haki wakati wote, kutoa uchambuzi kwa kujiamulia kutokana na hali ya mambo ya sahihi au isiyo ya sahihi, na siku zote inafanya kazi yake ya kiujenzi ya kuzishawishi Ukraine na Russia zifanye mazungumzo.
Lakini upande husika umelaumu upande wa China mara nyingi bila sababu yoyote.Marekani na nchi nyingine kadhaa zilisema kuwa China haichukui hatua halisi kwa ajili ya kutatua migogoro na pia haifuati hatua za nchi za magharibi za kuweka vikwazo kwa Russia, na Jumuiya ya washauri mabingwa ya Marekani ilisema kuwa mkakati wa China unaolenga kuweka uwiano katika pande mbili za migogoro haufanyi kazi hata kidogo.
Wakati Marekani inapolaumu mwingine, bora ijiangalie yenyewe kwanza. Ni nani aliyehimiza NATO ifanye upanuzi mara tano kwa upande wa mashariki? Ni nani aliyetia chumvi kuhusu hali wasiwasi na kusababisha kupamba moto kwa mgogoro? Katika suala la Ukraine, upande wa Marekani si mtazamaji asiye na makosa. Mtu anatia moto bila kusita, huku akilaumu mwingine kushindwa kuzima moto, kitendo chake hakika ni cha kutowajibika na ni kitendo cha aibu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma