Lugha Nyingine
Rais Xi awahamasisha “Wasamaria Wema wa China” kutoa ushawishi chanya kwa manufaa ya jamii
Rais Xi Jinping wa China Jumamosi alijibu barua kutoka Li Peisheng na Hu Xiaochun, wanaosifiwa kuwa “Wasamaria Wema wa China”, ambao wanafanya kazi kwenye eneo la utalii la Mlima Huangshan katika mkoa wa mashariki wa Anhui, akieleza matumaini yake kuwa wataendelea na kazi zao kama mifano ya kuigwa.
Kwenye barua yake Rais Xi amesisitiza kuwa umuhimu wa “Wasamaria Wema wa China” ni kwamba wafanyakazi hawa wa mashinani wamepata mafanikio yasiyo ya kawaida kwenye kazi zao za kawaida. Ameeleza matumaini yake kuwa wataendelea kuweka mifano ya kuigwa ili kutoa ushawishi chanya, kuwahamaisha watu walio karibu nao kufanya chochote wanachoweza kwa manufaa ya jamii na kuhimiza maadili makuu ya kijamaa. Rais Xi pia anatumai kuwa watawahamasisha watu walio karibu nao kuwa raia wema, wafanyakazi wazuri na wanafamilia wazuri, na kuchangia mchakato wa ustawishaji mkubwa wa taifa la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma