Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akagua Kikosi cha Jeshi la Majini Kamandi ya Kusini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba kwenye makao makuu ya Kikosi cha Jeshi la Majini la Kamandi ya Kusini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) Tarehe 11 Aprili 2023. (Xinhua/Li Genge)
ZHANJIANG, Guangdong - Rais Xi Jinping wa China Jumanne alikagua Kikosi cha Jeshi la Majini Kamandi ya Kusini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesisitiza kuimarisha mafunzo na utayari wa kupigana vita na kuharakisha mageuzi ili kuongeza viwango vya mambo ya kisasa vya jeshi hilo katika sekta zote.
Ametoa wito kwa vikosi vya majeshi kutekeleza kwa uthabiti majukumu waliyokabidhiwa na Chama na wananchi.
Kwenye makao makuu ya Kikosi cha Jeshi la Majini Kamandi ya Kusini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Rais Xi alikutana na wajumbe wa maofisa na wanajeshi na kupiga picha pamoja nao. Ameeleza kutambua mafanikio ambayo jeshi hilo limepata katika kujiboresha na kutekeleza majukumu yake tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012.
Rais Xi amesema vikosi vya jeshi vinapaswa kuchambua na kushughulikia masuala ya kijeshi kwa mtazamo wa kisiasa, kufanya mapambano ya kijeshi kwa uthabiti na kwa njia ya kunyumbulika, na kuongeza uwezo wa kuhakikisha majibu kwa wakati na sahihi katika hali ngumu.
Ameliagiza jeshi hilo kutetea kwa uthabiti mamlaka ya mipaka ya China na haki na maslahi ya baharini, na kujitahidi kudumisha utulivu wa jumla wa mikoa jirani ya China.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe wa maofisa na wanajeshi kwenye makao makuu ya Kikosi cha Majini Kamandi ya Kusini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Tarehe 11 Aprili, 2023. (Xinhua/Li Genge)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma