Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping apokea na kusikia ripoti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Macao SAR
Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkowa wa Utawala Maalum wa Macao ya China (SAR) Ho Iat Seng, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing, China, Desemba 18, 2023. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao wa China (SAR) Ho Iat Seng, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo amesikiliza ripoti kutoka kwa Ho juu ya hali ya sasa ya Macao na kazi ya serikali ya Macao SAR huku akipongeza kazi ya Ho katika mwaka uliopita.
Amesema Ho ameiongoza serikali ya Macao SAR katika kutekeleza majukumu yake kwa bidii, kushikilia mwelekeo wenye matokeo na kufanya kazi kwa bidii, kumaliza kwa mafanikio marekebisho ya Sheria ya Macao SAR ya Kulinda Usalama wa Nchi, na kuchukua hatua zenye utaratibu katika kuendeleza kazi ya kurekebisha sheria za mkoa kwa ajili ya kuchagua ofisa mtendaji wake mkuu na baraza la kutunga sheria.
Rais Xi pia ameeleza kuwa serikali ya Macao SAR imeimarisha usimamizi wa sekta ya michezo ya kubahatisha ya mkoa huo na kuandaa mpango wa kwanza wa pande zote wa Macao kwa ajili ya maendeleo yake mbalimbali.
Rais Xi amesema, mafanikio mapya yamepatikana katika kuendeleza ujenzi wa eneo la ushirikiano wa pande zote la Guangdong-Macao huko Hengqin, na mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa umepanuliwa zaidi, na Macao imepata ufufukaji wa haraka wa kiuchumi huku ikidumisha maelewano na utulivu wa kijamii.
Serikali Kuu ya China, itafanya kama kawaida, kutekeleza kikamilifu, kwa uthabiti na kwa usahihi sera ya "nchi moja, mifumo miwili", na sera ya "wazalendo kusimamia Macao," Rais Xi amesema.
Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao wa China (SAR) Ho Iat Seng, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing, China, Desemba 18, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma