Lugha Nyingine
Mkutano mkuu wa mwaka wa Bunge la Umma la China wafungwa
Viongozi wa China Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wakihudhuria kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, China, Machi 11, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING – Mkutano mkuu wa mwaka wa Bunge la Umma la 14 la China umefungwa siku ya Jumatatu ambapo viongozi wa China Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kikao cha kufungwa kwa mkutano huo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano huo, aliongoza kikao hicho cha kufungwa kwa mkutano kilichohudhuriwa na wajumbe 2,900 wa bunge hilo la umma.
Mkutano huo umepitisha Sheria ya marekebisho mapya kuhusu muundo wa vyombo na utaratibu wa kazi wa Baraza la Serikali la China. Rais Xi Jinping ametia saini amri ya rais kutangaza sheria hiyo.
Mkutano huo umepitisha ripoti ya kazi ya serikali na ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Mahakama ya Juu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China.
Mkutano huo umepitisha ripoti ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2023 na ripoti kuhusu mswada wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2024, na mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2024 umepitishwa kwenye mkutano huo.
Pia mkutano huo umepitisha ripoti ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kuu na za serikali za mitaa kwa Mwaka 2023 na ripoti juu ya mswada wa bajeti ya serikali kuu na za serikali za mitaa kwa Mwaka 2024, na bajeti ya serikali kuu kwa Mwaka 2024 imepitishwa.
Akihutubia kikao hicho cha mkutano, Zhao Leji amesema mkutano huo mkuu wa mwaka umekamilisha ajenda zake kwa mafanikio. Matokeo ya mkutano huo yamedhihirisha nguvu kubwa za demokrasia ya umma ya mchakato mzima ya China na mfumo wa kimsingi wa kisiasa wa nchi ya China, amesema.
Zhao ameeleza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na ni mwaka muhimu kwa kutimiza malengo ya mpango wa 14 wa maendeleo ya uchumi na jamii. Zhao amewataka wajumbe kuchukua hatua kwa kuendana na dhana ya maendeleo yanayotoa kipaumbele kwa manufaa ya watu, kuendeleza demokrasia ya umma ya mchakato mzima, na kuchangia maendeleo ya China.
Zhao, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, aliongoza mkutano wa tume ya wenyeviti na mkutano wa wenyeviti watendaji wa mkutano huo siku ya Jumatatu kabla ya kikao hicho cha kufungwa kwa mkutano mkuu.
Kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing , Machi 11, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China akiongoza mkutano wa nne wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Machi 11, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa tume ya wenyeviti wa mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akiongoza mkutano wa tatu wa viongozi watendaji wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma