Lugha Nyingine
Je umewahi kuona barua ya chuma cha pua ya kukubaliwa ombi la kujiunga na chuo kikuu?
Hivi majuzi, barua ya chuma cha pua ya kukubaliwa ombi la kujiunga na chuo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing, China imeshangaza watu wengi mtandaoni. Barua hiyo inatumia chuma cha pua maalumu ambacho ni kama karatasi, ikiwa na unene kama karatasi ya kawaida ya A4. Kampuni ya Shougang Jingtang ndiyo kampuni ya kuzalisha chuma cha pua hicho "chuma cha pua cha bawa la nyenje."
Chuma cha pua cha aina hii siyo tu inatumiwa kuzalisha barua za kukubaliwa maombi ya kujiunga na chuo, bali pia kadi za posta za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, kadi za salamu, stempu... Idadi ya bidhaa za kitamaduni zinazotumia "chuma cha pua cha bawa la nyenje" inaendelea kuongezeka, na imegeuza mtazamo wa asili wa watu kuhusu "chuma cha pua."
"Chuma cha pua cha bawa la nyenje" ni chuma cha pua chembamba zaidi kilichotengenezwa kwa pamoja na timu ya utafiti wa teknolojia ya Shougang na timu ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing. Inatumiwa hasa katika vipokeaji vya mawimbi vya vituo vya 5G na vifaa vingine mbalimbali vya kiteknolojia.
Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya chuma cha pua ya China imeingia katika hatua mpya ya mageuzi na maboresho kutoka kuwa kubwa hadi imara. Viwanda vya chuma cha pua vya jadi ya China vimeharakisha mageuzi yao ya kuwa kisasa na kuboresha ufanisi wa uzalishaji na ubora wa bidhaa kwa kutumia vifaa na teknolojia za otomatiki, kama vile data kubwa na akili mnemba.
(Picha inatoka video.)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma