超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Rais Xi atoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 60 ya UNCTAD

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2024

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye   hafla ya sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa  Baraza la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), Juni 12, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), Juni 12, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwa njia ya video siku ya Jumatano kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) ambapo ameeleza kuwa katika miaka hiyo 60 iliyopita tangu kuanzishwa kwake, kwa kufuata dhamira ya kufikia ustawi kwa wote, baraza hilo limehimiza kwa nguvu ushirikiano wa Kusini-Kusini, kutetea mazungumzo ya Kaskazini-Kusini, kuhimiza kujenga utaratibu mpya wa uchumi wa kimataifa, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya biashara na maendeleo ya kimataifa.

Rais Xi amesema kuwa Dunia ya sasa inapitia mabadiliko ya kasi ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, na amani na maendeleo vinakabiliwa na changamoto mpya, pande zote lazima zibebe majukumu yao kwa historia na watu, kuendelea na mwelekeo sahihi, na kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi ametoa wito kwa pande zote kujenga mazingira ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya amani. Na nchi zote, hasa nchi kubwa, zinapaswa kufuata ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kutetea Dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu, kufuata nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono Baraza la Biashara na Maendeeleo la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuonesha umuhimu wao mzuri zaidi.

Rais Xi amesema, pande zote zinapaswa kufuata mwelekeo wa maendeleo ya ufunguaji mlango, kutetea utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa kwa wote na jumuishi, kuhimiza biashara na uwekezaji huria na wa kirahisi, kutatua ipasavyo hali ya maendeleo isiyo ya uwiano, na kufanya mfumo wa usimamizi wa kimataifa uendelee kwa mwelekeo wa kuwa wa haki na usawa zaidi.

Rais Xi pia amesema kuwa pande zote zinahitaji kutumia fursa ya kihistoria ya kupata maendeleo kwa kutegemea uvumbuzi. Alisema ni muhimu kujenga mazingira ya uchumi wa kidijitali yaliyo ya ufunguaji mlango, jumuishi na yasiyo ya kibaguzi, kushikilia kanuni ya kutoa vipaumbele kwa watu, AI kwa wema na kuimarisha sheria na usimamizi husika wa AI ndani ya mfumokazi wa Umoja wa Mataifa, kuendeleza kikamilifu kufanya juhudi za uhamaji wa kuelekea maendeleo ya kijani, na kusaidia nchi nyingi zaidi zinazoendelea kujiunga na mwelekeo wa maendeleo ya teknolojia za kidijitali, za kisasa na za kijani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha