Lugha Nyingine
Mkutano wa Baraza la ustaarabu wa Dunia wafunguliwa Nishan, China
Picha hii iliyopigwa tarehe 10 Julai 2024 ikionyesha mwonekano wa ukumbi wa mkutano wa 10 wa Baraza la Nishan kuhusu Ustaarabu wa Dunia huko Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Xinhua/Guo Xulei)
JINAN –Mkutano wa 10 wa Baraza la Nishan kuhusu Ustaarabu wa Dunia umeanza siku ya Jumatano huko Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China ukiwa na mada ya Utamaduni wa Jadi na Ustaarabu wa zama tulizo nazo. Mkutano huo unalenga kutoa ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto dhidi ya Dunia na kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.
Mkutano huo utafanyika kwa siku mbili huko Qufu, alikozaliwa Confucius, mwanafalsafa mashuhuri wa China. Mkutano huo wa 10 wa Baraza hilo umevutia wageni karibu 400 kutoka nchi na maeneo 63, wakishiriki katika shughuli mbalimbali zikiwemo mahojiano ya ngazi ya juu, hotuba kuu, na majadiliano sambamba.
Baraza hilo pia lina mada ndogo sita, zinazohusu “mawasiliano kati ya ustaarabu mbalimbali na kufundishana chini ya Changamoto zinazoikabili Dunia. Kwa mara ya kwanza, baraza hilo linajumuisha jukwaa la utamaduni wa michezo na kongamano la utamaduni wa familia. Pia litaandaa mazungumzo kati ya China na Italia zenye ustaarabu tangu zama za kale.
Baraza la Nishan kuhusu Ustaarabu wa Dunia linaangazia mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali wa Dunia na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Baraza hilo linajumuisha midahalo ya kitaaluma, mazungumzo ya kimataifa na ya wazi kama jukwaa la kubadilishana mawazo kuhusu utamaduni wa kimataifa na dhana na fikra mbalimbali.
Wageni wakihudhuria kwenye mkutano wa 10 wa Baraza la Nishan kuhusu Ustaarabu wa Dunia huko Qufu, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Guo Xulei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma