Lugha Nyingine
Kenya kuvutia wawekezaji wa China katika bustani ya kijani ya viwanda
(CRI Online) Julai 23, 2024
Kenya inajizatiti kuvutia wawekezaji kutoka China kuanzisha shughuli zao katika eneo maalum la kijani la viwanda lililoko Naivasha, umbali mfupi kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda nchini Kenya, Abubakar Hassan Abubakar ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua jijini Nairobi, kuwa eneo hilo maalum la viwanda liko kwenye maeneo ya jotoardhi, ambayo ni chanzo endelevu na thabiti cha nishati.
Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa uwekezaji wa China katika sekta za uchumi wa kijani, ikiwemo sekta ya uzalishaji umeme kwa jua na uchakataji wa taka kwa ajili ya matumizi ya mzunguko.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma