Lugha Nyingine
Xi Jinping aongoza mkutano kuhusu kudhibiti mafuriko na kutoa msaada
BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameongoza mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC siku ya Alhamisi kwa kujadili na kupanga kazi zinazohusu udhibiti wa mafuriko na kutoa msaada.
China imeingia katika kipindi kigumu cha udhibiti wa mafuriko, ambapo mafuriko makubwa yanatazamiwa kutokea kwenye maeneo muhimu ya Mto Changjiang na Mto Manjano. Zaidi ya hayo, kuanza kwa vimbunga kunaweza kufanya hali ya udhibiti wa mafuriko kukabiliwa na changamoto na utatanishi zaidi, mkutano huo umesema.
Nchini China, kipindi cha kuanzia mwishoni mwa Julai hadi mapema Agosti ni msimu wa kilele wa mafuriko. Katika kipindi hiki, mvua kubwa na vimbunga husababisha kuinuliwa kwa viwango vya maji, na hivyo kuwa tishio kubwa kwa jamii zilizo kando ya mito, karibu na maziwa na pwani.
Utabiri wa hali ya hewa unaonesha kuwa, maeneo saba makubwa ya mitiririko ya mito nchini China huenda kukumbwa na mafuriko katika kipindi hicho. Zaidi ya hayo, vimbunga vinaweza kufika katika maeneo ya bara, vikiambatana na kuongezeka kwa matukio mabaya ya hali ya hewa na iliyopitiliza, ambayo inaweza kuleta matokeo mabaya ya balaa.
Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa cha China kimetoa tahadhari nyekundu, ambayo ni ya daraja la juu zaidi, kwa kimbunga Gaemi siku ya Jumatano. Hii ni mara ya kwanza kwa tahadhari hiyo nyekundu kutolewa kwa kimbunga mwaka huu.
Mkutano huo umezitaka mamlaka husika katika ngazi zote za serikali kuwa macho na kufanya juhudi kwa hiari na makini katika kudhibiti mafuriko ili kushinda vita kali dhidi ya mafuriko.
Mkutano huo umesisitiza sera ya kutoa kipaumbele kwanza kwa usalama wa maisha ya watu, umetoa agizo la kufanya kila juhudi kwa iwezekanavyo ili kupunguza madhara ya maisha ya watu na kuwahamishia maeneo salama mara moja wale wote walio hatarini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma