Lugha Nyingine
Tanzania kuwa mwenyeji wa mazoezi ya manuva ya kijeshi pamoja na?China katika kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa nchi hizo mbili
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazoezi ya manuva ya kijeshi pamoja na China baadaye wiki hii, kufuatia kuwasili kwa meli tatu za kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).
Mazoezi hayo ya manuva yatafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na pia uhusiano kati ya PLA na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi la Tanzania (JWTZ).
Wanajeshi wa China watashiriki kwenye mafunzo ya pamoja na JWTZ, yakijumuisha operesheni mbalimbali za kijeshi, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.
Kamanda wa Kikosi cha Majini cha JWTZ , Ameir Ramadhan Hassan, ameeleza matumaini yake kuhusu mazoezi hayo, akiyaelezea kuwa ni fursa ya mabadilishano ya ujuzi na uzoefu kati ya wanajeshi wa nchi hizo mbili.
Amesema wanatarajia kuwa mazoezi hayo yataimarisha uwezo wa kijeshi wa Tanzania na kukuza uhusiano wa karibu na Jeshi la Ukombozi wa Umma la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma