超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria aonya dhidi ya wageni kuingilia maandamano ya kupinga gharama za maisha

(CRI Online) Agosti 08, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Tuggar ametoa wito kwa balozi za nchi za nje kuepuka kuingilia maandamano yanayoendelea nchini humo ya kupinga gharama za maisha, akisema serikali inafanya kazi kwa bidii kushughulikia masuala ya raia.

Tuggar ametoa wito huo siku ya Jumatano wakati akizungumza katika mkutano na wajumbe wa mabalozi mjini Abuja, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa usaidizi wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kuhakikisha maisha bora kwa Wanigeria ndani na nje ya nchi.

Amesema wakati serikali inaendelea kujitahidi kufanya mageuzi mbalimbali ili kutatua changamoto zinazoikabili Nigeria na Wanigeria, ni kawaida kwamba hakuna taifa linalovumilia kuingiliwa na mataifa ya kigeni katika masuala yake ya ndani, akisisitiza kuwa nchi hiyo inaongozwa na utawala wa sheria na serikali itafanya kila iwezalo kulinda raia wake.

Ameonya kuwa serikali itachukua hatua zinazofaa dhidi ya taasisi yoyote ya kigeni iliyopo Nigeria, ambayo itabainika kuwa inaunga mkono moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja waandamanaji kwa njia zozote au kutaka kuingilia masuala ya ndani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha