Lugha Nyingine
Waziri wa usalama wa umma wa China akutana na maofisa wa Serbia na Afrika Kusini
Mjumbe wa Kitaifa ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Serbia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Ivica Dacic, ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano ujao wa 2024 wa Jukwaa la Ushirikiano wa Usalama wa Umma Duniani (Lianyungang) mjini Beijing, China, Septemba 8, 2024. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Mjumbe wa Kitaifa ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong amekutana na Naibu Waziri Mkuu wa Serbia ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Ivica Dacic na Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini Senzo Mchunu mjini Beijing siku ya Jumapili.
Kweye mkutano wake na Dacic, Wang ameeleza matumaini yake kuwa pande zote mbili zitachukua makubaliano muhimu ya wakuu wa nchi hizo mbili kama mwongozo, kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu katika kusimamia utekelezaji wa sheria, na kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa utekelezaji wa sheria katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa uhamiaji, mapambano dhidi ya uhalifu wa ulaghai wa simu na ugaidi.
Kwa upande wake Dacic amesema Serbia inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na ina nia ya kuzidisha ushirikiano na China katika masuala ya usimamizi wa utekelezaji wa sheria na usalama, na kusukuma uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya.
Katika mazungumzo yake na Mchunu, Wang amesema China ina nia ya kutekeleza kwa pamoja maoni muhimu ya pamoja ya viongozi wa nchi hizo mbili na Afrika Kusini, kuimarisha ujenzi wa mfumo wa mawasiliano kwenye ngazi ya juu, kuimarisha ushirikiano katika kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka, kujenga kwa pamoja uwezo wa utekelezaji sheria kuhusu usalama wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kulinda kithabiti maslahi ya pamoja, na kujenga kizuizi imara cha usalama kwa uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na ushirikiano kati ya China na Afrika.
Kwa upande wake Mchunu amesema urafiki kati ya Afrika Kusini na China una historia ndefu na kwamba Afrika Kusini inapenda kufanya ushirikiano wenye matokeo halisi na ufanisi wa polisi na China, kulinda ipasavyo usalama wa raia, taasisi na miradi mikubwa ya China nchini Afrika Kusini, na kusukuma uhusiano wa karibu wa Afrika Kusini na China.?
Mjumbe wa Kitaifa ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong akikutana na Naibu Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini Senzo Mchunu, ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano ujao wa 2024 wa Jukwaa la Ushirikiano wa Usalama wa Umma Duniani (Lianyungang) mjini Beijing, China, Septemba 8, 2024. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma