Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China ahimiza kampuni za nchi za nje?kushiriki katika maendeleo yenye sifa bora?ya China
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihutubia hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China (CIFIT) mjini Xiamen, Mkoani Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Septemba 8, 2024. (Xinhua/Wei Peiquan)
XIAMEN – Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng Jumapili alipohutubia hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China (CIFIT), katika mji wa Xiamen, Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China alihimiza kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa kigeni kushiriki katika maendeleo yenye sifa bora ya China, na kutafuta fursa zaidi za biashara katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Naibu Waziri Mkuu huyo amesema, yakiwa ni jukwaa muhimu la kuendeleza ushirikiano wa wazi kwa njia ya uwekezaji wa pande mbili, maonyesho hayo yamekuwa ya kimataifa na maalum zaidi, akiongeza kuwa maendeleo ya Maonyesho ya CIFIT ni ushahidi wa wazi wa kuendelea kwa juhudi za China kufungua mlango zaidi kwa dunia.
He ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema ili kufungua ukurasa mpya katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, China itashikilia sera ya msingi ya kufungua mlango, na kuongeza uwezo wake wa kufungua mlango huku ikipanua ushirikiano wa kimataifa, na kujenga mfumo mpya wa uchumi wazi katika ngazi ya juu.
Amesema kuwa China inahimiza maendeleo yenye sifa bora, kuharakisha maendeleo ya nguvu kazi mpya zenye sifa bora, kutekeleza zaidi mkakati wa maendeleo yanayoendeshwa na uvumbuzi, kuunga mkono uvumbuzi kwa njia zote, na kuendeleza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, akiongeza kuwa juhudi hizi zitasaidia kuunda nafasi pana ya soko na mazingira bora ya biashara kwa kampuni za kigeni.
Ameeleza matumaini yake kuwa kampuni zinazowekezwa kwa mtaji wa nje zitakuwa wadau wazuri wa kushiriki katika maendeleo yenye sifa bora ya China, wahamasishaji wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine, na wawezeshaji wa hadithi za kweli kuhusu mageuzi na ufunguaji mlango wa China kwa dunia ili kutafuta fursa zaidi za biashara na kupata maendeleo bora zaidi katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma