Lugha Nyingine
Wang Yi atoa wito kwa nchi za BRICS kushughulikia kwa pamoja matishio dhidi ya usalama
(CRI Online) Septemba 13, 2024
Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya mambo ya nje ya China, Bw. Wang Yi Jumatano alitoa wito kwa nchi za BRICS kushikana mikono katika kushughulikia matishio dhidi ya usalama katika mkutano wa ngazi ya juu.
Bw. Wang amesema, katika kukabiliana na changamoto za sasa za kiusalama, nchi za BRICS zinapaswa kuwa na mtazamo wa muda mrefu, kuonyesha mtazamo wa uwazi zaidi, na kushirikiana kwa karibu zaidi kushughulikia matishio dhidi ya usalama kwa pamoja, na kuingiza nishati chanya katika dunia yenye msukosuko na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga dunia ya amani na usalama.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma