超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

China yafungua vituo 12 vya utafiti wa nyuklia kwa wanasayansi wa kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2024

Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa tarehe 5 Desemba 2021 ikionyesha sehemu ya Maabara ya Utafiti ya chini ya ardhiya Beishan katika Mkoa wa Gansu, kaskazini-magharibi mwa China. (Picha na Wang Ju/Xinhua)

VIENNA - China itafungua vifaa 12 vya utafiti na majukwaa ya majaribio ya nyuklia kwa wanasayansi na taasisi za kimataifa ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, Liu Jing, makamu mwenyekiti wa Shirika la Nishati ya Atomiki la China (CAEA), amesema siku ya Jumatatu kwenye mkutano pembezoni mwa mkutano mkuu wa mwaka wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).

Liu amesema vifaa na majukwaa hayo ya nyuklia yatakayofunguliwa kwa wanasayansi wa kimataifa ni pamoja na Kinu cha Nyuklia cha Utafiti wa Hali ya Juu cha China, kifaa cha kizazi kipya cha tokamak Huanliu-3, na Maabara ya Utafiti ya chini ya ardhi ya Beishan.

Vifaa na majukwaa hayo ya nyuklia yanahusu maeneo kama vile utafiti wa kimsingi wa nyuklia, uzalishaji wa isotopu, kuigiza mazingira halisi ya nyuklia, majaribio ya vifaa, na kusafisha na kutupa taka za nyuklia.

Mkutano huo wa Jumatatu, wenye kaulimbiu ya "Kunufaisha Maendeleo," uliandaliwa na CAEA ili kuendeleza ushirikiano wa kimataifa katika utafiti na uendelezaji wa teknolojia ya nyuklia, wakati ambapo China inaadhimisha miaka 40 tangu ijiunge na IAEA.

Mwenyekiti wa kundi la kampuni za viwanda vya Nyuklia la China Yu Jianfeng amesema katika mkutano huo kuwa kampuni yake inalenga kuzidisha ushirikiano na IAEA na kupanua ushirikiano wa kimataifa.

Ameeleza matumaini yake kuwa kufungua vifaa vya utafiti wa nyuklia vya China utasaidia maendeleo ya teknolojia ya nyuklia duniani.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Mikhail Chudakov amnepongeza mafanikio makubwa ya China katika maendeleo ya nishati ya nyuklia na kusisitiza uhusiano wa muda mrefu na wenye matunda kati ya IAEA na CAEA.

Akikaribisha uamuzi huo wa China wa kufungua vifaa vyake zaidi vya utafiti na uendelezaji wa nyuklia, Chudakov amesema hatua hiyo itaimarisha zaidi uwezo wa kiufundi wa shirika hilo kusaidia nchi wanachama wake.

Picha hii iliyopigwa Agosti 10, 2023 ikionyesha eneo la kuunganisha sehemu kuu ya kinu cha kwanza cha kibiashara cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia, Linglong One, katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wali ya Changjiang, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Shirika la Taifa la Nyuklia la China/kupitia Xinhua)

Li Song (kulia, mbele), mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), akizungumza kwenye mkutano maalum wa Bodi ya Magavana wa IAEA mjini Vienna, Austria, Aprili 11, 2024. (Ujumbe wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa huko Vienna//kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha