超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Ndege ya C919 iliyoundwa?na China kwa kujitegemea yawasili Mkoa wa Xizang kwa mara ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2024

Ndege ya abiria ya C919 inayoendeshwa na Shirika la Ndege la China Southern ikipaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou Baiyun siku ya Alhamisi, ikiashiria safari ya kwanza ya kibiashara ya ndege hiyo ya C919 katika Mji wa Guangzhou. (Xinhua)

SHANGHAI - Ndege ya abiria ya C919 ya kuundwa China, iliyoundwa na Shirika la Ndege la Kibiashara la China (COMAC), imekamilisha safari ya kutoka Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China hadi Mkoa unaojiendesha wa Xizang siku ya Alhamisi, ikiashiria kutua kwa mara ya kwanza kwa ndege hiyo katika mkoa huo.

Mwisho wa safari hiyo ya ndege ya majaribio, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lhasa Gonggar, uko katika Bonde la Mto Yarlung Zangbo, kwenye mwinuko wa mita 3,569. Ukiwa umezungukwa na milima mikali, mazingira magumu na hali mbalimbali za hewa za eneo hilo zinaweka mahitaji ya juu kwa uendeshaji wenye ufanisi katika kuruka kwa ndege kwenye mwinuko wa juu.

Ndege hiyo ya C919 sasa itafanyiwa utafiti na majaribio ya safari za ndege kwa baadhi ya mifumo muhimu kama vile udhibiti wa mazingira, mifumo wezeshi ya usafiri wa anga na udhibiti wa mgandamizo na kani ambao ni muhimu kwa uendeshaji wa kwenye mwinuko wa juu, pamoja na ukaguzi wa uhimilivu kwenye viwanja vya ndege vya uwanda wa juu.

Hii inatarajiwa kuweka msingi wa kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa njia za anga za miinuko ya juu na uundaji wa hali mbalimbali za mwinuko wa juu kwa ndege katika siku zijazo, imesema COMAC.

Viwanja vya ndege vilivyo na mwinuko wa mita zaidi ya 2,438 juu ya usawa wa bahari vinajulikana kama viwanja vya ndege vya uwanda wa juu, wajuzi wa sekta hiyo wanasema.

Ndege ya abiria ya C919 (R) ikiwa imeegeshwa karibu na ndege ya ARJ21 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lhasa Gonggar huko Lhasa, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha