超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Tanzania yawahakikishia wazalishaji viwandani umeme wa uhakika

(CRI Online) Septemba 29, 2024

Serikali ya Tanzania imewahakikishia wazalishaji viwandani kuwa kutakuwa na umeme wa uhakika kusaidia uzalishaji wa ndani wa viwanda.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania Bw. Doto Biteko amesema Tanzania sasa ina umeme wa kutosha baada ya hivi karibuni kuongezwa umeme kutoka kwenye Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Bw. Biteko ametoa kauli hiyo wakati wa Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Wazalishaji Tanzania (TIMEXPO) 2024, kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Amesema licha ya masuala madogo madogo yaliyojitokeza katika miezi ya hivi karibuni, ambayo yalisababisha kukatika kwa umeme, uzalishaji wa umeme unaotokana na maji kwa sasa umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na hivyo kupunguza utegemezi wa gesi katika uzalishaji wa umeme.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha