Lugha Nyingine
Rais Biden atuma pongezi kwa Rais Xi kwa maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa PRC
BEIJING - Rais wa Marekani Joe Biden ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais wa China Xi Jinping katika maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC), msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema jana Jumamosi.
Viongozi wa nchi na vyama vingi vya siasa na wakuu wa mashirika ya kimataifa hivi karibuni wametuma ujumbe au barua za pongezi kwa Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), katika maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa PRC.
Msemaji huyo amethibitisha kuwa Rais Biden ni miongoni mwa viongozi wanaoipongeza China.
Kwenye ujumbe wake huo, Rais Biden amesema "kwa niaba ya watu wa Marekani, ninatuma salamu zetu za pongezi kwako na kwa watu wa Jamhuri ya Watu wa China mnaposherehekea miaka 75 tangu kuanzishwa kwake."Mimi na watu wa Marekani tunawasilisha salamu zetu za kutakia kila la kheri kwa watu wa Jamhuri ya Watu wa China," kwa mujibu wa msemaji huyo.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma