Lugha Nyingine
China yatoa wito wa juhudi zaidi katika kuboresha usimamizi wa dunia na kukabiliana na ukiukaji wa haki wa kihistoria uliofanywa kwa Bara la Afrika
Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong ametoa wito wa kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia na kushughulikia ukosefu wa haki wa kihistoria uliofanywa kwa Bara la Afrika.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano kati ya Shirika hilo na Umoja wa Afrika (AU), Balozi Fu amesema nchi za Afrika zimeibuka kutoka utawala wa kikoloni na kujipatia uhuru wa kitaifa, na uanachama wao umeleta mageuzi na kupanua kidhahiri ujumuishi wao katika Umoja wa Mataifa.
Balozi Fu amesema, wakati wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la 79 la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki iliyopita, viongozi wa Afrika walitoa wito wa kuongeza kasi ya mageuzi ya mfumo wa uongozi wa kimataifa ili kuondoa ukosefu wa haki wa kihistoria ambao Afrika imeteseka nao kwa muda mrefu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma