Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kuimarisha maendeleo ya Mkoa wa Xinjiang
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang (XPCC) huko Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Tarehe 7 Oktoba 2024. (Xinhua/Li Xiang)
URUMQI – Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng Jumatatu katika mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang (XPCC) huko Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang amehimiza juhudi za kuimarisha XPCC ili kuendeleza maendeleo ya Xinjiang.
He ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), aliongoza ujumbe wa serikali kuu ya China kwenda mkoani Xinjiang kushiriki kwenye shughuli hii.
Akiwa amekasimiwa na Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, He ametoa pongezi na salamu kwa watu wa makabila mbalimbali wa kikosi hiki kwa niaba ya serikali kuu.
Barua ya pongezi iliyotumwa na Kamati Kuu ya CPC, Baraza la Serikali la China na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ilisomwa kwenye mkutano huo.
Kikosi cha uzalishaji na ujenzi cha Xinjiang kilianzishwa Mwaka 1954 na askari waliokamilisha muda wao jeshini na kuanza kazi mkoani Xinjiang, na katika miongo saba iliyopita kikosi hiki kimetoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya Xinjiang, kuimarisha mshikamano wa makabila na utulivu wa kijamii, vilevile kulinda mipaka, barua hiyo iliyotumwa imeeleza.
He amesema kikosi hiki kimeanzisha njia mpya ya kujenga mashamba ya uzailishaji ili kupata maendeleo chini ya mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China katika miaka 70 iliyopita.
Watu wa kizazi hadi kizazi wa kikosi hiki wamefanya juhudi kubwa za kujitolea mihanga na kutoa mchango mkubwa, na wamekusanya uzoefu mwingi muhimu, Naibu Waziri Mkuu huyo amesema.
Ametoa wito kwa kikosi hiki kutumia ipasavyo nguvu zake katika kudumisha utulivu na kulinda maeneo ya mpaka ili kuhudumia utulivu wa kijamii wa Xinjiang, kuunda vichocheo vipya vya kiviwanda na vya sayansi na teknolojia ili kuhimiza maendeleo yenye sifa bora, na kutumia mageuzi na ufunguaji mlango kujenga mkoa huo kuwa "mkondo wa dhahabu" kati ya Asia na Ulaya na mnara wa ufunguaji wa upande wa magharibi wa China.?
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang (XPCC) huko Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Tarehe 7 Oktoba 2024. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma