超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Setilaiti ya China kwenye anga ya juu yafanya majaribio ya modeli kubwa ya AI

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2024

Roketi ya kubeba satalaiti ya Smart Dragon-3 iliyobeba satalaiti nane ikiruka kutoka baharini karibu na mji wa Haiyang Mkoani Shandong mashariki mwa China, Septemba 24, 2024. (Picha na Guo Houze/Xinhua)

Roketi ya kubeba setilaiti ya Smart Dragon-3 iliyobeba setilaiti nane ikiruka kutoka baharini karibu na mji wa Haiyang Mkoani Shandong mashariki mwa China, Septemba 24, 2024. (Picha na Guo Houze/Xinhua)

BEIJING - ADA Space, kampuni ya teknolojia ya mtandao wa intaneti ya setilaiti ya AI ya China, imetangaza siku ya Jumapili kwamba setilaiti yake iliyorushwa hivi karibuni imekamilisha uthibitisho wa kiufundi wa teknolojia ya modeli kubwa ya AI wakati wa ufanyaji kazi ya obiti kwenye anga ya juu.

Kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 5, setilaiti hiyo ilifanya majaribio 13 ya muundo wake mkubwa wa AI, ikihusisha aina nyingi za maswali ya uelekezaji chini ya hali mbalimbali za uendeshaji na joto.

Jaribio hilo la kiufundi limethibitisha uwezo wa kuendana na hali halisi ya anga ya juu wa modeli hiyo kubwa ya AI ya kampuni hiyo kwenye obiti, kutegemewa kwa jukwaa la setilaiti la mifumo ya kompyuta, na uwezo wa mifumo ya kompyuta yenye ufanisi mkubwa wakati wa ufanyaji kazi kwenye anga ya juu, kampuni hiyo imesema.

Katika hatua inayofuata, setilaiti hiyo itafanya utoaji wa data ya 3D ya kuhisi kwa mbali katika obiti kwa kutumia teknolojia ya AI. Uwezo wake wa upigaji picha za 3D za AI unaweza kusaidia aina mbalimbali za programu pacha za kidijitali katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na shughuli za uchumi kwenye anga ya chini, utalii wa kitamaduni na michezo.

Setilaiti hiyo ilirushwa kwa roketi ya kubeba setilaiti ya Smart Dragon-3 kutoka baharini karibu na mji wa Haiyang Mkoani Shandong mashariki mwa China Septemba 24.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha