超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Bunge la Ethiopia lamteua waziri wa mambo ya nje kuwa rais mpya

(CRI Online) Oktoba 08, 2024

Mabunge mawili ya Ethiopia yamemteua Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Taye Atske Selassie kuwa rais mpya.

Uteuzi huo unafuatia kumalizika kwa muhula wa rais wa sasa Sahle-Work Zewde, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka sita.

Rais huyo mpya aliyeteuliwa ameapishwa siku ya Jumatatu mbele ya wajumbe wa Mabaraza ya Ehiopia ya Wawakilishi wa Umma na lile la Shirikisho kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Akiwa na uzoefu wa kidiplomasia kwa muda wa miongo mitatu, ikiwa ni pamoja na jukumu lake la kuwa mwakilishi wa kudumu wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa, Atske Selassie amekuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kuanzia Februari mwaka huu hadi uteuzi wake huo mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha