Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kuzidisha ushirikiano wa Jumuiya ya SCO
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 23 wa Bodi la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Islamabad, Pakistan, Oktoba 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)
ISLAMABAD - Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametoa wito wa kuendeleza kwa kina na kupanua ushirikiano ndani ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwenye Mkutano wa 23 wa Bodi la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa SCO uliofanyika siku ya Jumatano huko Islamabad, Pakistan.
Li amesema, jumuiya ya SCO ni jukwaa muhimu la kulinda amani na utulivu wa kikanda na kuhimiza maendeleo na ustawi wa nchi mbalimbali, na kwenye mkutano wa kilele wa Astana mwezi Julai, Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo walifikia maoni muhimu ya pamoja juu ya kujenga kwa pamoja maskani yenye mshikamano na kuaminiana, amani na utulivu, ustawi na maendeleo, ujirani na urafiki mwema, vilevile haki na usawa.
Ili kujenga maskani ya pamoja kama hiyo, kunahitaji msingi thabiti zaidi wa kisiasa, uhakikisho wa usalama wa kutegemeka zaidi, uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi, kiunganishi cha kihisia na ushirikiano wa pande nyingi wa uratibu mzuri zaidi, amesema Waziri Mkuu.
Amesema, China inapenda kujiunga pamoja na pande zote katika kubadilisha maoni ya pamoja yaliyofikiwa na wakuu wa nchi zao kuwa vitendo vyenye matokeo mazuri na kubadilisha mawazo kuwa hali halisi juu ya kujenga maskani ya pamoja yenye mshikamano na kuaminiana, amani na utulivu, ustawi na maendeleo, ujirani na urafiki mwema, pamoja na haki na usawa.?
Li ametoa mapendekezo manne ya kuendeleza kwa kina ushirikiano wa jumuiya ya SCO. Kwanza, kuimarisha hali ya kuunganisha kimkakati kulingana na dhamira na majukumu, pili, kupanua ushirikiano wenye matokeo halisi kulingana na mahitaji ya maendeleo, tatu, kuweka mkazo katika kufuatilia hatari kubwa na kufanya juhudi za kukabiliana nazo, na nne, kuitikia matarajio ya watu ya kupanua mawasiliano ya kitamaduni.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 23 wa Bodi la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Islamabad, Pakistan, Oktoba 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma