Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana kukomesha madhara ya ukoloni
Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Geng Shuang amesema, China inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kujikita katika madhara ya ukoloni, kuyaondoa na kulinda usawa na haki za kimataifa, na kuhimiza kuanzisha utaratibu wa kimataifa wa haki zaidi.
Akizungumza katika mjadala wa Kamati ya 4 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondoa madhara ya ukoloni uliofanyika jana Jumatano, Balozi Geng amesema China inakaribisha Azimio la kuondoa madhara ya aina zote za ukoloni lililopitishwa na Kamati Maalum ya Kuondoa Ukoloni, na inatarajia azimio hilo litapitishwa katika Kamati ya 4 ya Baraza Kuu.
Pia amesema China inatoa wito kwa nchi ambazo zinaendeleza mfumo wa kikoloni au kunufaika nao kuonyesha utashi wa kisiasa, kubeba majukumu ya kihistoria, kufidia madhara ya ukoloni, kuacha kufuata fikra za kikoloni, kuacha umwamba, kuacha kudhuru maslahi ya nchi nyingine, na kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma