超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Moldova yafanya uchaguzi wa rais, kura ya maoni ya kujiunga na?EU

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2024

Raia wa Moldova wanaoishi Romania wakiwa kwenye foleni kupiga kura nje ya kituo cha kupigia kura mjini Bucharest, Romania, Oktoba 20, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

Raia wa Moldova wanaoishi Romania wakiwa kwenye foleni kupiga kura nje ya kituo cha kupigia kura mjini Bucharest, Romania, Oktoba 20, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

BUCHAREST - Wapiga kura wa Moldova wamepiga kura jana Jumapili kwa ajili ya uchaguzi wa rais na kura ya maoni ya nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya (EU) ambapo Tume Kuu ya Uchaguzi (CEC) ya Moldova imesema siki hiyo katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba vituo vya kupigia kura 2,219 vilifunguliwa kwa wapigakura ambao wanakadiriwa kufika milioni 3.3 kuanzia saa 1 Asubuhi (0400 GMT) hadi 3 usiku kwa saa za huko (1800 GMT).

Uchaguzi huo unafuatiliwa na waangalizi 2,061, wakiwemo waangalizi wa kitaifa 1,277 na waangalizi 784 wa kimataifa, CEC imesema.

Chini ya katiba ya nchi hiyo, mgombea lazima apate kura nyingi kwa zaidi ya nusu ya wapigakura wote ili kumwezesha kuchaguliwa kuwa rais; vinginevyo, wagombea wawili walio na kura nyingi zaidi wanaendelea na duru ya pili.

Mbali na kuchagua rais, wapiga kura pia watapiga kura ya maoni kuhusu iwapo lengo la kujiunga na Umoja wa Ulaya linapaswa kuandikwa katika katiba ya nchi hiyo.

"Kura yetu kwenye kura ya maoni ndiyo itakayoamua hatma yetu kwa miongo mingi ijayo," amesema Maia Sandu, rais aliyeko madarakani wa Moldova anayewania muhula wa pili madarakani.

Tangu kuchaguliwa kwake Mwaka 2020, Sandu amekuwa akiiongoza Moldova kuelekea mshikamano zaidi na EU. Aliongoza nchi hiyo kufikia hadhi ya mwombaji wa uanachama wa EU Mwaka 2022. Mwezi Juni Mwaka 2024, mazungumzo rasmi ya kujiunga na EU yalianzishwa.

Raia wa Moldova wanaoishi Romania wakipiga kura zao kwenye kituo cha kupigia kura mjini Bucharest, Romania, Oktoba 20, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

Raia wa Moldova wanaoishi Romania wakipiga kura zao kwenye kituo cha kupigia kura mjini Bucharest, Romania, Oktoba 20, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha