Lugha Nyingine
Tamasha la 45 la Filamu la Kimataifa la Cairo laanza, upande wa China washiriki
Waigizaji wa filamu na wageni wakipiga picha kwenye zulia jekundu ya ufunguzi wa Tamasha la 45 la Filamu la Kimataifa la Cairo (CIFF) nchini Misri, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
CAIRO - Tamasha la 45 la Filamu la Kimataifa la Cairo (CIFF) limeanza Jumatano jioni katika Jumba la Opera la Cairo Misri, upande wa China umeshiriki kwenye tamasha hilo, ambapo nyota mkongwe wa filamu wa Misri Hussein Fahmy, ambaye pia ni mwenyekiti wa tamasha hilo, ameeleza kufurahia uwepo wa filamu kutoka China kwenye tamasha hilo.
"Tuna wageni 18 wa China leo na filamu saba za China zinazoshiriki katika CIFF ya 45. Tumekuwa tukivutiwa na filamu za China, na nimetazama filamu za China tangu nilipokuwa mwanafunzi katika Chuo kikuu cha Filamu," Fahmy ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye zulia jekundu wakati wa hafla ya ufunguzi wa tamasha.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati yetu na China unaweza kuleta filamu zitakazopigwa kwa pamoja siku zijazo, akisema kuwa CIFF ilisaini makubaliano ya maelewano (MoU) na Shirika Kuu la Radio na Televisheni la China (CMG) mwishoni mwa Julai, ambayo yanatilia maanani zaidi kufanya ushirikiano katika kupiga filamu za kimataifa, kubadilishana mawazo kuhusu ujuzi wa usanii na utamaduni, na kunufaika pamoja na wageni waheshimiwa, filamu, na majaji wa kitaalamu.
Moja kati ya filamu za China zinazoshiriki katika tamasha hilo ni "Historia fupi ya Familia", iliyoongozwa na Lin Jianjie, filamu hiyo pomoja na filamu nyingine saba zimeshiriki kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Wiki ya Majaji.
Tamasha hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1976, limekuwa tamasha la mwaka la filamu ambalo limefanyika kwa miaka mingi na kutambuliwa na dunia ya nchi za Kiarabu, Afrika, na Mashariki ya Kati. Tamasha hilo la mwaka huu linafanyika kuanzia Tarehe 13 hadi 22 Novemba.
Nyota wa filamu wa Misri Hussein Fahmy (Kulia), ambaye pia ni mwenyekiti wa tamasha hilo, akipiga picha kwenye zulia jekundu ya ufunguzi wa Tamasha la 45 la Filamu la Kimataifa la Cairo (CIFF) Misri, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Mwigizaji wa filamu akitembea kwenye zulia jekundu kwa ajili ya hafla ya ufunguzi wa Tamasha la 45 la Filamu la Kimataifa la Cairo (CIFF) Misri, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Nyota wa filamu wa Misri Hussein Fahmy (Kulia), ambaye pia ni mwenyekiti wa tamasha hilo, akipiga picha kwenye zulia jekundu ya ufunguzi wa Tamasha la Kimataifa la 45 la Filamu la Cairo (CIFF) mjini Cairo, Misri, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma