Lugha Nyingine
Kenya yathibitisha wagonjwa wapya watano wa ugonjwa wa mpox huku ufuatiliaji ukiimarishwa
Wizara ya Afya ya Kenya imethibitisha wagonjwa wapya watano wa mpox, na kufanya jumla ya wagonjwa kufikia 28 katika kaunti 12 za nchi hiyo.
Waziri wa Afya Deborah Barasa amesema Jumanne kuwa juhudi za ufuatiliaji na kuzuia zinaendelea kote nchini, akiwataka Wakenya kuendelea kuwa macho na kuzingatia hatua za kuzuia.
Katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, Barasa amesema wagonjwa hao wapya waliothibitishwa ni pamoja na watatu kutoka kaunti ya Nakuru magharibi mwa Kenya na wawili kutoka kaunti ya Mombasa katika mkoa wa pwani.
Amebainisha kuwa jumla ya watu 204 waliokutana ana kwa ana na wagonjwa hao wametambuliwa, kati yao 147 wamekamilisha kipindi hitajika cha ufuatiliaji cha siku 21.
Ameongeza kuwa watu wanane kwa sasa wako chini ya usimamizi, wawili wamejiweka karantini na 17 wamepona kabisa, pia tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mtu mmoja ameripotiwa kufariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma