Lugha Nyingine
Kampuni ya ujenzi ya China yasisitiza dhamira kwa Tanzania katika ripoti ya CSR
DAR ES SALAAM - Kampuni ya Reli na Uhandisi ya Jianchang ya China (CRJE) (Afrika Mashariki) nchini Tanzania imetoa ripoti yake ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) Jumatatu, ikisisitiza dhamira yake ya kuwa shirika linalowajibika na kutoa mchango kwa ushirikiano unaokua kati ya Tanzania na China.
Ripoti hiyo ya CSR imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian, Mwenyekiti wa kampuni ya CRJE Jiang Yuntao, Mkurugenzi wa Ukuzaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania John Mnali pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku. .
Jiang amesema, kampuni ya CRJE siku zote imeshikilia wazo la "kujenga miradi bora," pamoja na ushiriki wake katika ujenzi wa Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), mradi unaoonyesha urafiki kati ya China na Tanzania.
Amesema, kwa miaka mingi CRJE imewekeza dola za Marekani zaidi ya milioni 260 katika ujenzi wa miradi, kutoa mafunzo ya kiufundi kwa wafanyakazi wenyeji, kuunga mkono maendeleo ya jamii, kulinda mazingira na kutekeleza majukumu yake ya kijamii ya kampuni.
“Ripoti ya leo ya CSR siyo tu kuakisi kazi tuliyofanya huko nyuma bali pia ni ahadi ya kuendelea kutoa mchango katikamaendeleo ya Tanzania,” amesema Jiang.
CRJE imeshajenga miradi mikubwa 200 nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na Daraja la Nyerere jijini Dar es Salaam, ukumbi wa mijadala wa Bunge la Tanzania katika mji mkuu Dodoma, kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere mkoani Pwani. .
Shoma Phillip Ndono, afisa mwandamizi aliyemwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Damas Ndumbaro amesema CRJE imeongeza urafiki kati ya Tanzania na China kupitia miradi ambayo imeboresha hali ya maisha ya wananchi wa Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma