Lugha Nyingine
Panda mmoja ‘atoroka gerezani’ kwenye Bustani ya Wanyama ya Beijing
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 17, 2021
Mchana wa Desemba 15, Panda anayeitwa Menglan alipanda mwenyewe kwenye eneo ambalo liko nje ya uwanja wake wa michezo, na hali hiyo iliwavutia watalii wengi kutazama. Kwa bahati nzuri, eneo hilo lilitengwa na watalii, na mfugaji alitumia chakula kumrubuni panda huyo ili arudi kwenye banda lake, na hali ya panda ilikuwa nzuri kama ya kawaida. Bustani ya Wanyama ya Beijing ilisema itakarabati haraka iwezekanavyo uwanja huo wa panda.
Wafanyakazi wa bustani hiyo walisema, ingawa panda ana uzito mkubwa, lakini ni mwepesi sana, na siku zijazo uwanja wake wa michezo utafanyiwa ukarabati ili kutompa Panda Menglan na panda wengine nafasi ya kujihatarisha.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma