Lugha Nyingine
Rais Xi asema China iko tayari kuwasilisha Michezo ya Olimpiki iliyo rahisi, salama na murua (2)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amemwambia Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) Thomas Bach ambaye yuko ziarani nchini China kuwa China iko tayari kuwasilisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi iliyo rahisi, salama na murua.
Xi amekutana na Bach, kwenye Jumba la Wageni la Taifa la Diaoyutai mjini Beijing, siku 10 kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Michezo hiyo mnamo Februari 4.
Katika mkutano huo, Xi amesema "kila kitu kiko tayari" kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing.
Akibainisha kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Mwaka 2022 ni tukio la kwanza la kimataifa la mashindano mengi kufanyika kama ilivyopangwa tangu kuzuka kwa janga la UVIKO-19, Xi amesema kuwa ni mafanikio ya utendaji wa kauli mbiu mpya ya Olimpiki ya "Haraka zaidi, Juu zaidi, Nguvu zaidi -–Kwa Pamoja."
Amesema kuwa katika kuandaa michezo hiyo, China imepata uungwaji mkono siyo tu kutoka kwa watu wa China, bali pia kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Rais Xi, karibu wanamichezo 3,000 kutoka takriban nchi na kanda 90 watashiriki mashindano ya Beijing 2022, ambayo yanahusisha michezo mingi zaidi na itatoa medali nyingi za dhahabu kuliko michezo yoyote ya awali ya majira ya baridi, ikiwa ni fursa kwa wanamichezo wengi zaidi kutimiza ndoto zao.
Ameongeza kwamba, China ina imani ya kuhakikisha usalama wa washiriki wote wa Michezo hiyo, wafanyakazi husika na watu wa China.
Xi amesema, kufanyika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto huko Beijing Mwaka 2008, Michezo ya Olimpiki ya Vijana huko Nanjing Mwaka 2014 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya 2022 kumeleta shauku ya Wachina kwa michezo ya Olimpiki, kuhimiza maendeleo ya michezo nchini China na kuchukua jukumu muhimu katika kukuza moyo wa Olimpiki kote duniani.
Amebainisha kwamba, Wazo la "Pamoja" lililochangiwa na Michezo ya Olimpiki, linahitajika zaidi kuliko hapo awali.
"Badala ya kupanda katika boti ndogo 190 tofauti, nchi zote duniani zinapaswa kukaa pamoja katika meli moja kubwa na kusafiri kuelekea mustakabali mzuri zaidi, na hii ndiyo sababu tulikuja na "Pamoja kwa mustakabali wa Pamoja wa baadaye" kama kauli mbiu rasmi ya Beijing 2022," Xi amesema.
Kwa upande wake Bach huku akisema nchi nyingi zimepinga kuingiza siasa kwenye Michezo ya Olimpiki, ameishukuru China kwa kazi bora ya kufanya maandalizi ya Michezo hiyo, akisema kwamba amefurahishwa na kumbi za michezo zilizojengwa, hatua kamili za kukabiliana na UVIKO-19 na dhana ya kisasa ya maendeleo endelevu.
Bach ameonesha imani kamili kwamba hatua kali zinazochukuliwa na China zitahakikisha Michezo ya Olimpiki inafanyika kwa usalama, mafanikio bila changamoto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma