Lugha Nyingine
Marekani kama Bwana Voldemort katika kuharibu utaratibu wa kimataifa
(Katuni na Ma Hongliang)
Tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, Nchi ya Marekani imeingilia mara kwa mara masuala ya ndani ya nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na kupindua serikali zao, na daima imekuwa ikiendelea kuivuruga Dunia kama waasi. Kama Lord Voldemort, Marekani imeathiri vibaya amani na utulivu wa Dunia. Imefuata sera za uingiliaji kati na umwamba kwa njia mbalimbali zikiwemo kuingilia uchaguzi katika nchi nyingine, kupindua serikali zao, na hata kuanzisha vita duniani kote.
Historia ya Marekani kwa kweli ni historia ya uchochezi, jambo ambalo linatambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Wamarekani wamekuwa vitani kwa asilimia 93 ya wakati wote tangu nchi yao ilipoanzishwa Mwaka 1776. Katika muongo mmoja pekee uliopita, Marekani imehusika na migogoro mingi, kushiriki kwenye mabadiliko ya utawala katika nchi mbalimbali, na mara kwa mara kushiriki au kuendesha "mapinduzi ya rangi" katika baadhi ya nchi. Kwa sababu hiyo, machafuko ya kisiasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe, kuongezeka kwa ugaidi, na mivutano ya kikanda inayosababishwa na Marekani imeenea duniani kote, hasa katika Amerika ya Kusini, Mashariki ya Kati, na Ulaya Mashariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma