Lugha Nyingine
Xi Jinping asisitiza kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza malengo yaliyowekwa na Mkutano Mkuu wa CPC
YAN'AN - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Alhamisi amesisitiza kuhimiza moyo mkuu wa kuanzishwa kwa Chama na moyo wa Yan'an, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza malengo na majukumu yaliyowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.
Xi, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amewaongoza Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi, wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, katika safari ya kuelekea hadi Yan'an, kituo cha zamani cha mapinduzi katika Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China.
Kituo cha kwanza cha Xi na viongozi wengine siku ya Alhamisi kilikuwa eneo la Mkutano Mkuu wa 7 wa CPC.
Mkutano huo uliofanyika Mwaka 1945 ni wenye umuhimu mkubwa katika historia ya CPC, na kuashiria chama hicho kukomaa zaidi kisiasa, kiitikadi na katika mpangilio wake, Xi amesema.
“Kisiasa, Chama kizima kiliunganishwa chini ya bendera ya Mao Zedong, na kiitikadi, mwongozo wa kiuongozi wa Fikra Mao Zedong kwa Chama kizima ilianzishwa na Fikra Mao Zedong iliingizwa kwenye Katiba ya Chama,” Xi amesema.
Kituo kilichofuata cha ziara yao hiyo kilikuwa makazi ya zamani ya Mao Zedong na wanamapinduzi wengine wa kizazi kikongwe ambapo hapo alitoa hotuba ya utangulizi kuhusu jinsi wimbo maarufu wa mapinduzi "Mashariki Kwekundu " ulivyoandikwa na kuwa maarufu.
Baada ya hapo, Xi na viongozi wengine walifika kwa gari kwenye Ukumbi wa Kumbukumbu za Mapinduzi ya Yan'an kutembelea maonyesho ya miaka 13 ya Kamati Kuu ya CPC huko Yan'an.
Kuanzia Mwaka 1935 hadi 1948, Mpaka wa Shaanxi-Gansu-Ningxia, ambao Yan'an ilikuwa kitovu, ulikuwa makao makuu ya Kamati Kuu ya CPC. Ilitumika kama kitovu cha mwongozo wa kisiasa katika Vita vya Kupinga Uvamizi wa Japani, na eneo la jumla la kusukuma mbele mapambano ya ukombozi ya watu wa China.
Katika hotuba muhimu aliyoitoa baada ya kutembelea maonyesho hayo, Xi amepongeza Yan'an kama eneo takatifu la mapinduzi ya China na chimbuko la China Mpya. Ameeleza kuwa ni mjini Yan'an ambapo Kamati Kuu ya Chama na wanamapinduzi wakongwe, akiwemo Mao Zedong, waliongoza mapinduzi ya China kutoka katika hali ya chini hadi kufikia hatua ya mabadiliko ya kihistoria, na kubadilisha matarajio ya China.
Xi amesema aliishi na kufanya kazi Yan'an kwa miaka saba, na baba yake pia aliwahi kufanya kazi Yan'an.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma