Lugha Nyingine
Xi Jinping akagua Kituo cha Komandi cha Operesheni za Pamoja cha CMC, asisitiza mafunzo kwa askari, utayari wa kupigana
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne amekagua Kituo cha Komandi cha Operesheni za Pamoja cha Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akionyesha msimamo wa CMC mpya kuhusu kutekeleza mipango na malengo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kuimarisha mafunzo kwa askari na utayari wa kupigana.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, Mwenyekiti wa CMC, na Kamanda Mkuu wa Kituo cha Komandi cha Operesheni za Pamoja cha CMC, amesema jeshi lote linapaswa kujitolea nguvu zake zote na kutekeleza kazi zake zote kwa utayari wa mapigano, kuongeza uwezo wake wa kupigana na kushinda, na kutimiza vyema misheni na majukumu yake katika zama mpya.
Alipowasili kwenye kituo hicho cha komandi siku ya Jumanne takriban saa 10:00 alasiri, Xi alipewa maelezo mafupi.
Baadaye, alikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa kituo cha komandi na kutoa salamu za dhati kwa wafanyakazi wake wote. Baada ya hapo, alipiga picha pamoja na wajumbe hao.
Xi ameviagiza vikosi vya jeshi kusoma kwa kina, kueneza na kutekeleza mipango na malengo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kuchukua hatua madhubuti za kuboresha ulinzi wa kitaifa na kijeshi.
Huku akiweka bayana kuwa Dunia inapitia mabadiliko makubwa zaidi ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, Xi amesisitiza kuwa usalama wa taifa wa China unakabiliwa na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu na kutokuwa na uhakika, na kazi zake za kijeshi bado ni ngumu.
Ameagiza vikosi vyote vya jeshi kutekeleza mawazo ya Chama juu ya kuimarisha jeshi kwa zama mpya, kufuata mkakati wa kijeshi kwa zama mpya na kuzingatia ufanisi wa kupambana kama kigezo pekee.
Xi pia amewaagiza kulinda kwa uthabiti mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, na kukamilisha kwa ufanisi kazi mbalimbali zilizokabidhiwa na Chama na wananchi.
“Kituo cha komandi, ambacho hutoa msaada muhimu kwa amri za kimkakati za Kamati Kuu ya CPC na CMC, ni muhimu sana na kinabeba majukumu mazito,” Xi ameeleza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma