Lugha Nyingine
Simulizi ya Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Sanamu ya Shaba Inayoonesha Vituo vya Acupuncture Kwenye Ngozi ya Mwili wa Mtu
Kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani huko Geneva, Uswisi, kuna sanamu ya shaba ya kuonesha alama za vituo vya Acupuncture kwenye ngozi ya mwili wa mtu, kimo cha sanamu hiyo ni cha mita 1.8. Sanamu hii ya shaba inayowakilisha matibabu ya jadi ya China ya tiba ya Acupuncture ni zawadi iliyoletwa na Rais wa China Xi Jinping alipotembelea WHO Januari 18, 2017.
Sanamu hiyo ikiwa chombo cha kutoa mafunzo kuhusu matibabu ya jadi ya China ya kupiga sindano ya Acupuncture na kielelezo cha kutathmini uwezo wa madaktari, imekuwa alama ya elimu ya matibabu ya jadi ya China, na tiba ya Acupuncture pia imejumuishwa kwenye Orodha Wakilishi ya Utamaduni Usioshikika ya Urithi wa Binadamu.
Kwenye hafla ya kutoa zawadi hiyo, Rais Xi Jinping na Mkurugenzi Mkuu wa WHO wa wakati huo Margaret Chan, walifungua pazia kwa pamoja ili kuonesha sanamu hiyo ya shaba. Akitoa hotuba kwenye hafla hiyo, Rais Xi alisema, tunapaswa kurithi, kuendeleza na kutumia vizuri elimu ya matibabu ya jadi, na kuhimiza mafungamano ya elimu ya matibabu ya jadi na elimu ya matibabu ya kisasa kwa mtazamo wa wazi na jumuishi.
Kwa hivi sasa, matibabu ya jadi ya China na Dawa za Mitishamba za Kichina (TCM) vimeenea katika nchi na maeneo 196 duniani, na China imesaini makubaliano maalum ya ushirikiano wa TCM na serikali, mamlaka za kikanda na mashirika ya kimataifa zaidi ya 40.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma