Lugha Nyingine
Simulizi za Zawadi za Kitaifa za Rais Xi: Nakala ya "Maandishi ya Jiwe la Kumbukumbu ya Ziara ya Zheng He"
Septemba, 2014, Rais wa wakati huo wa Sri Lanka alimzawadia Rais Xi Jinping wa China nakala ya maandishi kwenye "Jiwe la Kumbukumbu ya Ziara ya Zheng He". (Picha na Hu Yang) |
Septemba 16, 2014, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya kiserikali nchini Sri Lanka. Rais wa wakati huo wa Sri Lanka alimzawadia Rais Xi nakala ya maandishi kwenye jiwe la kale , ambayo ni zawadi kubwa ya kitaifa iliyotolewa na nchi hiyo ya "Lulu ya Bahari ya Hindi" kwa kiongozi mkuu wa China.
Jiwe hilo la kumbukumbu lililowekwa nchini Sri Lanka kutokana na ziara ya Zheng He, baharia wa China katika zama za kale. Mwanzoni mwa Karne ya 15, Zheng He aliongoza kikosi cha merikebu kusafiri baharini na kufika Ceylon (yaani Sri Lanka ya leo) baada ya miezi kadhaa. "Katika safari yao, Zheng He na kikosi chake cha merikebu kila walipofika nchi moja waliweza kuweka jiwe moja lililochongwa maandishi ya kumbukumbu ya ziara yao. Na ziara ya Zheng He ilileta amani na ustawi badala ya vita." Mei 15, 2019, katika maonyesho ya mabaki ya kale ya kitamaduni yaliyofanyika kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mazungumzo kuhusu Ustaarabu wa Asia, Rais Xi Jinping alisimama karibu na mfano wa jiwe la kale na nakala ya maandishi kwenye jiwe hilo, akiitambulisha kwa viongozi wa nchi nyingine mbalimbali.
Mwaka 2013, China na Sri Lanka zilikuwa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati, na pia Sri Lanka ilikuwa nchi ya kwanza ambayo serikali yake ilitoa taarifa rasmi ya kuunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Mwaka 2016, kwa mara ya kwanza China ilikuwa mshirika wa kibiashara na mwagizaji mkubwa zaidi wa bidhaa za Sri Lanka. Mwaka 2019, Mradi wa ujenzi wa Mji Mpya wa Bandari ya Colombo, ambao uliwekezwa na kujengwa na kampuni za China, ulikamilisha kazi ya kuziba maji ya bahari kwenye eneo la hekta 269 ili kupanua ardhi kwenye mji wa bandari…
Watu wa Sri Lanka walisema, tofauti na nchi nyingine, msaada wa China unakuja bila masharti yoyote. Wakati nchi nyingi zilizoko nyuma kimaendeleo zilipokuwa ziko kwenye "pembe zilizosahauliwa" za utandawazi wa kiuchumi, Rais Xi Jinping amechora ramani kubwa ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na anakaribisha kwa dhati nchi mbalimbali duniani "kupanda treni ya mwendo kasi ya maendeleo ya China" ili watu wa nchi mbalimbali na wa rangi tofauti waweze kupata fursa za maendeleo na kunufaika kwa pamoja na matunda ya maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma