Lugha Nyingine
Daraja la kuvuka Mto Yangtze la Longtan likiendelea kujengwa huko Nanjing, China
Siku hizi Daraja la kuvuka Mto Yangtze (Changjiang) la Longtan lililoko Mkoa wa Jiangsu wa China limeingia hatua ya ujenzi wa kufunga nguzo za chuma cha pua, na linatarajiwa kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi Machi.
Daraja la kuvuka Mto Yangtze la Longtan kwa jumla linakadiriwa kuwa na urefu wa kilomita 5.8. Linajengwa kwa kiwango cha China cha barabara kuu ya mwendo kasi cha njia sita za kupitisha magari, likiwa na muundo wa kasi ya kilomita 100 kwa saa. Baada ya daraja hilo kukamilika, litakuwa na umuhimu mkubwa katika kuitikia mkakati wa maendeleo wa Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Yangtze wa China, kuboresha mpango wa njia za kuvuka Mto Yangtze, na kuboresha mtandao wa mawasiliano ya barabara kuu za mwendo kasi. (Picha na Fang Dongxu/Vip.people.com.cn)
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma