Lugha Nyingine
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China lafanya kikao cha kufungwa kwa mkutano wake mkuu wa mwaka
Kikao cha kufungwa kwa mkutano mkuu wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
BEIJING – Mkutano mkuu wa pili wa mwaka wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, kimefanya kikao chake cha kufungwa kwa mkutano huo leo Jumapili asubuhi ambapo Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wamehudhuria kikao hicho kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Mkutano wa kikao hiki umepitisha Azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, azimio la ripoti ya hali ya kushughulikiwa kwa mapendekezo yaliyotolewa na washauri wa kisiasa tangu mkutano mkuu wa awamu iliyopita, ripoti ya kuthibitishwa kwa mapendekezo mapya, na azimio la kisiasa juu ya mkutano mkuu wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa.
Wang Huning, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC, ametoa hotuba katika kikao hicho cha mkutano.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma