Lugha Nyingine
Video: Mimi ni Ustaarabu wa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2024
Ungeuliza,
Mimi ni nani?
Ni sanamu za ajabu za askari na farasi wa Enzi ya Qin,
au ni Panda wanaopendeza sana?
Ni utamaduni maridadi wa vitoweo mbalimbali,
au ni Kung Fu inayounganisha nguvu laini na nguvu thabiti?
Nilisikia majibu haya kwa mara zisizohesabika.
Lakini mimi ni zaidi ya hayo.
Mimi ni Mto Manjano unaobetabeta na Mto wa Yangtze unaokimbia kwa kasi.
Mimi ni moshi unaopaa kutoka jangwa kubwa, na ni manyunyu kusini mwa Mto Yangtze.
Mimi ni mambo mbalimbali yenye mvuto wa kushangaza na ni miujiza ya ufundi wa ajabu.
Mimi ni mpokeaji wa ushirikiano na tamaduni anuwai, pia nina shauku ya kujifunza kutoka ubora wa wengine.
Mimi ni Ustaarabu wa Taifa la China.
Ninatiririka na kukimbia kwenye ardhi ya China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma