Lugha Nyingine
Mtaa wa urefu wa Kilomita 1 waonesha “Uchumi wa Usiku” wa Hangzhou, China (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2024
Kazi za sanaa zilizotengenezwa kwa mikono zikivutia watalii kutazama kwenye soko la usiku la Wulin, tarehe 25, Mei. (Picha na Zhang Yongtao/People’s Daily Online) |
Mapema katika msimu wa joto, wakati anga linaanza kuwa giza, kando ya Barabara ya Wulin mjini Hangzhou, China, safu kadhaa za mabanda ya maduka huwekwa kwenye mtaa huo wenye urefu usiofikia kilomita 1, na wafanyabiashara wenye mabanda hayo hukaribisha wateja kwa shauku na ukarimu chini ya mianga mizuri ya taa, na “maisha mazuri ya usiku” ya Hangzhou yanaanza hapa.
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mji huo imetilia maanani sana maendeleo ya uchumi wa usiku na umezalisha kwa mafanikio mfululizo wa chapa za uchumi wa usiku kupitia uungaji mkono wa sera na uboreshaji wa mazingira ya biashara. Likiwa ni mfumo mpya wa biashara uliozalishwa kwenye eneo la biashara ya jadi, "Soko la usiku la Wulin” ni kivutio kipya cha uhai wa uchumi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma