超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Vitu zaidi ya 900 vya mabaki ya kale vyaopolewa kutoka kwenye meli iliyozama katika Bahari ya Kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 14, 2024
Vitu zaidi ya 900 vya mabaki ya kale vyaopolewa kutoka kwenye meli iliyozama katika Bahari ya Kusini mwa China
Picha hii ya kumbukumbu isiyo na tarehe ikionyesha chombo cha kuzamia chini ya bahari kinachoendeshwa na dereva cha Shenhai Yongshi (Shujaa wa Baharini) kikifanya kazi ya kuzamia baharini kufanya utafiti wa mabaki ya kale na uchunguzi kwenye bahari ya kina kirefu. (NCHA/ Xinhua)

HAIKOU – Idara ya Kitaifa ya Mabaki ya Kale ya Utamaduni ya China imesema jana Alhamisi kuwa, vitu zaidi ya 900 vya mabaki ya kale ya kitamaduni vimeopolewa kutoka kwenye meli mbili za kale zilizozama baharini ambazo ziligunduliwa katika Bahari ya Kusini.

Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mkoani Hainan, kusini mwa China umesema kuwa, uchimbuaji huo uliofanywa kutoka Mwaka 2023 hadi 2024, ni juhudi za pamoja za taasisi za utafiti na makumbusho ya eneo husika.

Vitu jumla ya 890 vya mabaki ya kale ya utamaduni vimechimbuliwa kutoka kwenye meli namba 1, ikiwa ni pamoja na vyombo vya kauri na vyombo vya ufinyanzi wa udongo, pamoja na sarafu za shaba. Kutoka kwenye meli namba 2, vitu 38 vya kale vimepatikana, ikiwa ni pamoja bidhaa za mbao, vyombo vya kauri, na vya ufinyanzi wa udongo, magamba ya konokono, na pembe za kulungu.

Oktoba 2022, meli mbili hizo za kale zilizozama za Enzi ya Ming (1368-1644) ziligunduliwa kwenye kina cha bahari cha mita takriban 1,500 karibu na mteremko wa kaskazini-magharibi wa Bahari ya China ya Kusini.

Ugunduzi huo unatoa ushahidi kwamba mababu wa zama za kale wa China walihuisha na kutumia eneo la bahari ya kusini na kusafiri kwenda na kurudi kwenye eneo hilo la bahari, na meli hizo mbili za kale zilizozama ni ushahidi muhimu wa biashara na mawasiliano ya kitamaduni kwenye Njia ya Kale ya Hariri ya Baharini, amesema Guan Qiang, naibu mkuu wa Idara ya Kitaifa ya Mabaki ya Kale ya Utamaduni ya China.

Guan amesema kuwa, utafiti wa mabaki ya kale na uchunguzi huo kwenye bahari ya kina kirefu unaofungamanisha sayansi na teknolojia ya bahari ya kina kirefu ya China, na utafiti wa mabaki ya kale chini ya maji, umeonesha kuwa utafiti wa China wa mabaki ya kale kwenye bahari ya kina kirefu umefikia kiwango cha juu duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha