Lugha Nyingine
Mkutano wa Dunia wa AI Mwaka?2024 juu ya usimamizi wa kimataifa wafunguliwa Shanghai, China (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024
Mkono wa roboti ukichukua mpira unaotumika kwenye mchezo wa mpira magongo kwenye Mkutano wa Dunia wa AI Mwaka 2024 mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Julai 4, 2024. (Xinhua/Wang Xiang) |
Mkutano wa Dunia wa AI Mwaka 2024 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa Kimataifa wa AI umefunguliwa mjini Shanghai, Mashariki mwa China siku ya Alhamisi.
Mkutano huo unajikita katika kaulimbiu isemayo "Kusimamia AI kwa Wema na kwa Wote" mwaka huu, kwa lengo la kuanzisha majukwaa ya kimataifa ya ushirikiano na mawasiliano yenye uwazi, ujumuishaji, na ushiriki sawa, kuendeleza usimamizi wa kimataifa wa AI, na kuanzisha mfumo wa usimamizi ulio wazi, wenye usawa na ufanisi.
Mkutano huo unawakutanisha pamoja maafisa wa serikali, na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viwanda, vyuo vikuu na taasisi za utafiti, miongoni mwa wengine. (Xinhua/Wang Xiang)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma