Lugha Nyingine
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Mashindano ya kwanza ya Kimataifa ya Boti za Matanga kwa Majeshi ya Majini yakifanyika Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini-Mashariki mwa China, Julai 24, 2024. (Picha na Li Haotian/Xinhua) |
DALIAN - Mashindano ya kwanza ya Kimataifa ya Boti za Matanga kwa Majeshi ya Majini, yaliyoandaliwa na jeshi la majini la China, yamemalizika siku ya Alhamisi huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, ambapo timu mbili kutoka Chuo cha Jeshi la Majini cha Dalian cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), pamoja na timu ya Jeshi la majini la Russia, zimekuwa washindi wa nafasi tatu bora za mbele kulingana na alama zao za jumla.
Timu jumla ya 16 za wanajeshi wa majini kutoka vyuo vya majeshi ya majini vinavyowakilisha China na nchi nyingine nane zikiwemo Brazil, Chile, Italia na Russia zilichuana kwenye mashindano hayo.
Shughuli nyingine mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo vya kijeshi, ziliandaliwa pamoja na mashindano ya kuhimiza mabadilishano kati ya vyuo vya vikosi vya majini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma