超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Rais Xi akutana na Waziri Mkuu wa Italia, atoa wito wa kushikilia moyo wa Njia ya Hariri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2024

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Julai 29, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni mjini Beijing siku ya Jumatatu, ambapo ameeleza kuwa China na Italia ziko kwenye ncha mbili za Njia ya Kale ya Hariri, mawasiliano ya kirafiki yenye historia ndefu kati ya nchi hizo mbili yametoa mchango mkubwa kwa mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu wa Mashariki na Magharibi, pamoja na maendeleo ya binadamu.

Rais Xi amesema, moyo wa Njia ya Hariri ulio wa amani na ushirikiano, ufunguaji mlango na ujumuishi, kufundishana na kuigizana, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ni mali ya pamoja ya China na Italia.

“Katika hali ya kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kasi ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, nchi mbalimbali ama zitapiga hatua kwa pamoja za maendeleo kwa kupitia mafungamano ya mawasiliano na mshikamano, au kurudi nyuma moja moja kwa kupitia kufunga milango na kufanya mafarakano" Rais Xi amesema huku akiongeza kuwa China na Italia zinapaswa kushikilia na kuenzi moyo wa Njia ya Hariri, kutendeana na kuendeleza uhusiano wa pande mbili kutoka kwa mtazamo wa kihistoria, ngazi ya kimkakati na kutupia macho siku za baadaye za muda mrefu, na kusukuma uhusiano wao kuendelezwa kwa hatua madhubuti.

Rais Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kuendelea kufuata desturi za mawasiliano ya kirafiki, na kuendelea kuelewana na kuheshimiana kwa njia za maendeleo za kila mmoja wao.

Rais Xi amesema China inaiunga mkono Italia katika kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi Mwaka 2026 na inatumai kuwa Italia itatoa hatua rahisi za visa kwa raia wa China wanaosafiri kwenda Italia.

Kwa upande wake Meloni amesema zikiwa nchi zenye ustaarabu wa kale, Italia na China kila upande unausifu upande mwingine na kujifunza kutoka kwa upande mwingine na kwamba hali ya hivi sasa ya kimataifa inakumbwa na mabadiliko makubwa, na China ikiwa ni nchi kubwa muhimu kubwa inatoa mchango usio na mbadala katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia nzima.

Pande hizo mbili zimetoa mpango kazi wa 2024-2027 kuhusu kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote.?

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Julai 29, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Julai 29, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha