超碰caoporen国产公开,亚洲男人在线天堂2019香蕉,国产精品对白刺激,九九热这里只有国产中文精品2

Deni la taifa la Marekani lazidi dola trilioni 35 kwa mara ya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2024

Picha iliyopigwa Oktoba 9, 2023 ikionyesha Ikulu ya Marekani huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Picha iliyopigwa Oktoba 9, 2023 ikionyesha Ikulu ya Marekani huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Jumla ya deni la umma la serikali kuu ya Marekani imepita dola za Kimarekani trilioni 35 kwa mara ya kwanza, kama ilivyorekodiwa mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani siku ya Jumatatu.

Jumla ya deni la umma lililopo imepanda hadi kufikia dola za Kimarekani trilioni 35 siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa Taarifa mpya ya Kila Siku ya Wizara ya Fedha ya Marekani iliyotolewa hivi karibuni. Takwimu hizo zilitolewa upya mwishoni mwa kila siku ya kazi kwa takwimu za siku ya awali ya kazi.

Miezi saba iliyopita, deni la taifa la Marekani lilizidi dola za Kimarekani trilioni 34 mwishoni mwa Desemba 2023. Miezi mitatu kabla ya hapo, Marekani ilifikia kiwango cha kihistoria kwa kuvuka dola za Kimarekani trilioni 33.

"Kukopa kunaendelea tu kwenda juu, bila kujali na bila kuzaa matunda," amesema Maya MacGuineas, Mkuu wa Kamati kwa ajili ya Bajeti ya Serikali Kuu inayowajibika, katika taarifa.

"Hata hivyo licha ya hatari na ishara zote za tahadhari ya hatari, kengele hizi za tahadhari zinaonekana kuangukia kwenye masikio ya viziwi." ameongeza.

Kwa mujibu wa Mfuko wa Peter G. Peterson, shirika lisiloegemea upande wowote wa chama cha siasa nchini Marekani linalolenga kushughulikia changamoto za muda mrefu za kifedha za Marekani, deni hilo la taifa la dola za Kimarekani trilioni 35.001 ni sawa na deni la dola za Kimarekani 103,945 kwa kila mtu nchini Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha